Manchester
United imeondoshwa katika Mashindano UEFA Champions League baada ya
kukubali kulala kwa jumla ya mabao 2-1 ikiwa Uwanja wake wa nyumbani,
Old Trafford, dhidi ya Sevilla kutoka Spain.
Mabao ya Sevilla yamefungwa na Ben Yedder katika ya 74 na 78 kipindi cha pili, huku bao la United likifungwa na Lukaku kwenye dakika ya 84.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Spain, timu hizo zilenda sare ya 0-0.
Matokeo hayo sasa yanaiondosha rasmi Manchester United kwenye michuano hii na inakuwa timu ya kwanza kutoka England kutolewa mashindanoni.

20:27:00
Rais
Donald Trump amefuta kazi Waziri wa wa Mambo ya Nje, Rex Tillerson na
amemteua Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) Mike Pompeo.
"Mike
Pompeo, ambaye ni mkurugenzi wa CIA, atakuwa waziri wetu wa mambo ya
nje. Atafanya kazi vizuri sana," amesema Trump kwa njia ya Twitter
Jumanne.
"Nakushukuru sana Rex Tillerson kwa huduma uliyoitoa!" ameongeza rais.
Shirika la Habari la CNN limesema nafasi ya Pompeo inatarajiwa kuchukuliwa na Gina Haspel.
Tillerson, Jumatatu alilazimika kukatisha ziara yake ya kwanza ndefu barani Afrika kwa kile kilichoelezwa kwamba kazi nyingi.
“Kutokana
na mahitaji katika ratiba ya waziri, anarudi Marekani mapema baada ya
kukamilisha ziara ya kiserikali Chad na Nigeria,” amesema msaidizi wake
Steve Goldstein.
Tillerson
aliyeanza ziara ya Afrika Jumatano alirudi Marekani baada ya kutembelea
Ethiopia, Djibouti na Kenya ambako ilielezwa aliugua kwa muda.
Kwa
mujibu wa CNN, Trump alimtaka Tillerson kujiuzulu nafasi hiyo tangu
Ijumaa wakati akiwa katika ziara ya nchi kadhaa za Afrika.
20:19:00
Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda maalum DSM, Lazaro Mambosasa amesema kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi, Abdul Nondo hakutekwa
. Aidha amesema uchunguzi umebainisha kuwa alikwenda Mkoani Iringa kwa mpenzi wake waliyekuwa wakiwasiliana muda wote wa safari.
“Polisi baada ya kupata taarifa hii tulianza ufuatiliaji ili kubaini ukweli, tulipokea taarifa kutoka jeshi la polisi Iringa kuwa Mwanafunzi huyo alipatikana mkoani humo wilaya ya Mafinga akiendelea na shughuli zake na wala hakuripoti mahali popote” -Mambosasa
Mambosasa amesema kuwa walipomkamata walikuwa na mashaka kuwa huenda akawa amepatwa na ugonjwa wa malaria ya kichwa iliyopelekea kufanya hayo na kudai kuwa alipelekwa hospitali na kupimwa na kuonekana kuwa mzima asiye na matatizo yoyote ya kiakili.

06:43:00
Baraza
la Wazee wa Chadema limemuomba Rais John Magufuli kukutana na wazee
ili kubadilishana nao mawazo sambamba na kumpa ushauri wa masuala
mbalimbali yanayoendelea nchini.
Akizungumza
leo Jumanne Machi 13, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam, katibu mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka amesema
kumekuwa na mambo mengi yanayopigiwa kelele, ni vyema rais akakutana na
wazee ili wamueleza mambo hayo.
“Ni
lazima kama Taifa tuchukue hatua mapema kabla hatujachelewa. Rais
Magufuli akubali kuitikia wito wa kukutana na wazee ambao watakuwa na
ujasiri wa kumshauri ili kuepusha Taifa kuingia kwenye majanga,”
amesema.
Amesema
suala la wazee kukutana na rais, kimekuwa ni kilio cha muda mrefu na
kwamba nchini Kenya viongozi wameweza kukaa meza moja na kumaliza
tofauti zao.
“Lazima
tukae tujue mustakabali wa Taifa hatuwezi kusema hakuna tatizo.
Tunamtaka akutane na wazee, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya
siasa tuzungumze kwa kuwa hii ni nchi yetu wote na si ya chama kimoja,”
amesema.
06:27:00
Pengo
la pointi tatu zilizokuwa zimesalia ili kuifikia Simba kileleni iliyo
nafasi ya kwanza kwenye ligi msimu huu hatimaye limezibika kufutia
ushindi wa Yanga dhidi ya Stand United jioni hii.
Ikicheza
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga imeibuka na ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya Stand United, na kuwafanya wafikishe pointi 46 sawa
na vinara Simba, ingawa wanasalia kileleni kutokana na faida ya mabao
mengi ya kufunga.
Alikuwa
ni Yusuph Mhilu aliyefanya kazi nzuri mapema dakika ya 6 ya mchezo,
kazi iliyosababisha beki wa Stand, Ally Ally kujifunga, kufuatia kupiga
krosi nzuri kulia mwa Uwanja na kuzaa bao.
Dakika
ya 11, kiungo aliyewahi kuichezea Simba, Ibrahim Ajib alifunga bao la
pili na kufanya ubao wa matokeo usome 2-0. Mpaka dakika 45 za kwanza
zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa mabao hayo mawili.
Kipindi cha pili kilipoanza, Stand walimiliki mpira kwa asilimia kubwa wakipambana kutafuta mabao, ambapo juhudi zao zilizaa matunda kwa Vitalis Mayanga kufunga katika dakika ya 83.
Ilichukua dakika mbili pekee Obrey Chirwa akaiandikia Yanga bao la 3 kwenye dakika ya 85 na kufanya mchezo uende mpaka dakika 90 na kumalizika, matokeo yakiwa ni mabao 3-1.
Matokeo hayo yameifanya Yanga ilingane kwa alama na vinara wa ligi, Simba, kwa kuwa na alama sawa ambazo ni 46, japo Simba wana mchezo mmoja mkononi.

10:35:00
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema
kuwa anapokea mialiko mingi kutoka nje ya nchi lakini amesema hawezi
kusafiri kwenda huko kwasababu sio jimbo lake.
Akiwa ametimiza siku 859 madarakani, Rais John Magufuli ametembelea nchi chache huenda kuliko watangulizi wake wanne.
Magufuli
ametembelea Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia katika kipindi chote cha
utawala wake huku akitimiza miaka miwili, miezi minne na siku saba tangu
aapishwe kuwa Rais wa Tanzania Novemba 5, 2015.
Huenda hilo lilimfanya jana atoe siri na sababu zinazomfanya asipende kusafiri mara kwa mara nje ya nchi.
Akiwa
mjini Singida jana alikozindua kiwanda cha mafuta ya kupikia cha Mount
Meru Millers Group, Rais Magufuli alisema amekataa zaidi ya mialiko 70
ya kwenda nje ya nchi kwa sababu hakuchaguliwa na Watanzania kwenda huko
bali kuwatumikia.
10:27:00