Askofu Gwajima Atoweka: Polisi wamtafuta kila kona bila mafanikio


Askofu Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima ametoweka ghafla wakati jeshi la polisi likiwa lina mtafuta usiku na mchana, jeshi la polisi liliweka kambi nyumbani kwa askofu huyo kwa takribani masaa saba hapo jana bila mafanikio ya kumuona askofu huyo kama ilivyoripotiwa na mpekuzi

kitendo hicho cha kutoweka kwa askofu Gwajima kimetokea baada ya kusambaa kwa audio amabayo inasemekana ni sauti yake akimtaka Rais magufuli aihame CCM kwa maaana kuna watu wanamhujumu

Naye kamanda wa jeshi la polisi  Simon Sirro kanda rasmi ya Dar es salaam ameelezea kwa nini walienda nyumbani kwa Gwajima bila kutoa taarifa na hatua ambazo jeshi hilo limechukua baada ya kumkosa

“Si lazima apelekewe taarifa, askari walikwenda kwa nia njema ya kuonana naye ndiyo maana hawakutoa taarifa,” alisema Sirro na kuongeza: “Kama amejificha, tukimbaini alipo tutamkamata na atambue bado tunamtafuta.” alisema Kamanda Simon Sirro

Lakini Gazeti la MWANANCHI  rimeripoti kua Askofu Gwajima ameenda Dubai. Hii si mara ya kwanza kwa askofu huyo kutafuta na jeshi la polisi baada ya kutoa kauli zenye utata.

0 comments:

Post a Comment