![]() |
| Suzan Lyimo |
Bunge la Tanzania limeawasimamisha wabunge wawili wa chama
cha Demokrasia na maendeleo Suzan Lymo na Anatrophia Theonest kutohudhuria
vikao vya bunge visivyozidi vitano kwa kusema uongo bungeni.
Uamuzi huo umetolewa leo na kiti cha spika baada ya
mapendekezo ya kamati ya bunge ya haki, maadili na madaraka ya bunge
kupendekeza kuwa wabunge hao wapewe adhabu hiyo baada ya kubainika ni kweli waliliambia
bunge uongo kwa nyakati tofauti.
Akisoma mapendekezo hayo makamu mwenyekiti wa kamati ya haki
, maadili na madaraka ya Bunge Mh. Almas Maige amesema kuwa wabunge hao
walidanganya bunge kwa kuwashutumu Mh. Hamad Yusuf Masauni aliyeshutumiwa na Suzan
Lyimo Pamoja William Lukuvi aliyeshutumiwa na Anatrophia Theonest na wote
walioshutumu wamebainika na kamati kuwa wamesema uongo.
Uongo unaotajwa kusemwa na wabunge hao uko kama ifuatavyo...
Kuhusu Suzan Lyimo…
Inadaiwa kuwa Mhe. Suzan Lyimo (Mb) alipokuwa akichangia alitoa kauli kwamba, kuna magari 777 ya washawasha ya polisi yameingizwa nchini, taarifa za uhakika alizonazo kama Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ni kwamba, magari ya washawasha yaliyonunuliwa ni 32 tu na sio 777 yaliyotajwa na Mhe. Susan Lyimo.
Kuhusu Anatropia, Mh maige amesema ..
“Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 4 Februari, 2016 Mhe.
William Lukuvi (Mb) Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwasilisha
katika Meza ya Spika katika Ukumbi wa Bunge barua ya malalamiko akilalamikia
kuwa mnamo 3 Februari, 2016 katika Mkutano wa Pili, Kikao cha Saba, Bunge la
Kumi na Moja wakati wa majadiliano kuhusu Kamati ya Mipango, Mhe. Anatropia
Theonest wakati alipokuwa akichangia kuhusu Kamati ya Mipango alisema uongo
Bungeni kwa kudai kuwa yeye Mhe.
Lukuvi, akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mwaka 2011
alihusika na uporaji wa viwanja walivyopewa waathirika wa mabondeni na kwamba
jambo hilo kweli kwa kuwa Mwaka 2011, Mhe. Lukuvi hakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam bali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na
Bunge.”

0 comments:
Post a Comment