Mhe Lissu amesema kuwa upasuaji huo utafanyika tarehe 14 Machi, 2018
katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg ambako amekuwa
akitibiwa tangu mwezi Januari.
Wapendwa wangu, Naomba niwape taarifa ya maendeleo yangu ya kiafya. Ninaendelea vizuri na matibabu. Mguu wa kulia unaendelea kupata nguvu na sasa ninaweza kusimama kwa miguu yote bila msaada wa magongo. Hata hivyo, timu ya madaktari bingwa wa mifupa wanaonitibu, wamenitaarifu kwamba kasi ya mfupa wa juu ya goti kuunga ni ndogo sana. .
“Madaktari wangu wamesema kwamba wasipoingilia kati na kurekebisha mfupa huo, kwanza, itachukua muda mrefu sana kuunga; na pili, hata ukiunga baada ya huo muda mrefu, hautaunga kwa namna itakayoondoa hatari ya kuvunjika siku za mbeleni. Kwa sababu hizi, madaktari wangu wamependekeza kufanya operesheni nyingine kwenye mfupa wa juu ya goti la kulia. Hivyo, siku ya Jumatano ijayo ya tarehe 14 March, 2018, nitarudi Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg, kwa ajili ya kufanyiwa operesheni hiyo,“ameeleza Mhe Tundu Lissu kwenye taarifa yake.

0 comments:
Post a Comment