Rais Magufuli Afunguka sababu za kuto safiri mara kwa mara nchi za Nje

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa anapokea mialiko mingi kutoka nje ya nchi lakini amesema hawezi kusafiri kwenda huko kwasababu sio jimbo lake.

Akiwa ametimiza siku 859 madarakani, Rais John Magufuli ametembelea nchi chache huenda kuliko watangulizi wake wanne.

Magufuli ametembelea Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia katika kipindi chote cha utawala wake huku akitimiza miaka miwili, miezi minne na siku saba tangu aapishwe kuwa Rais wa Tanzania Novemba 5, 2015.

Huenda hilo lilimfanya jana atoe siri na sababu zinazomfanya asipende kusafiri mara kwa mara nje ya nchi.

Akiwa mjini Singida jana alikozindua kiwanda cha mafuta ya kupikia cha Mount Meru Millers Group, Rais Magufuli alisema amekataa zaidi ya mialiko 70 ya kwenda nje ya nchi kwa sababu hakuchaguliwa na Watanzania kwenda huko bali kuwatumikia.

0 comments:

Post a Comment