Pengo
la pointi tatu zilizokuwa zimesalia ili kuifikia Simba kileleni iliyo
nafasi ya kwanza kwenye ligi msimu huu hatimaye limezibika kufutia
ushindi wa Yanga dhidi ya Stand United jioni hii.
Ikicheza
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga imeibuka na ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya Stand United, na kuwafanya wafikishe pointi 46 sawa
na vinara Simba, ingawa wanasalia kileleni kutokana na faida ya mabao
mengi ya kufunga.
Alikuwa
ni Yusuph Mhilu aliyefanya kazi nzuri mapema dakika ya 6 ya mchezo,
kazi iliyosababisha beki wa Stand, Ally Ally kujifunga, kufuatia kupiga
krosi nzuri kulia mwa Uwanja na kuzaa bao.
Dakika
ya 11, kiungo aliyewahi kuichezea Simba, Ibrahim Ajib alifunga bao la
pili na kufanya ubao wa matokeo usome 2-0. Mpaka dakika 45 za kwanza
zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa mabao hayo mawili.
Kipindi cha pili kilipoanza, Stand walimiliki mpira kwa asilimia kubwa wakipambana kutafuta mabao, ambapo juhudi zao zilizaa matunda kwa Vitalis Mayanga kufunga katika dakika ya 83.
Ilichukua dakika mbili pekee Obrey Chirwa akaiandikia Yanga bao la 3 kwenye dakika ya 85 na kufanya mchezo uende mpaka dakika 90 na kumalizika, matokeo yakiwa ni mabao 3-1.
Matokeo hayo yameifanya Yanga ilingane kwa alama na vinara wa ligi, Simba, kwa kuwa na alama sawa ambazo ni 46, japo Simba wana mchezo mmoja mkononi.

0 comments:
Post a Comment