Tanzania kuanza kutumia lugha ya kiswahili katika mikutano yake ya kimaataifa


Serikali ya Tanzania inatarajia kuanza kutumia lugha ya Kiswahili katika mikutano ya kimataifa .taarifa hiyo imetolewa wakati wazir mkuu Mhe Kassim Majaliwa alipokua anajibu maswali ya papo kwa papo bunge hapo jana

Lugha ya kiswahili ni miongoni mwa lugha kubwa  barani Afrika ikitumiwa na watu zaidi ya milioni 100

 Mhe Zainabu Vulu(ccm) aliuliza ni namna gani serikali inenzi lugha ya Kiswahili iliyotumiwa na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika u kuunganisha taifaletu  na inatumiaje fursa ya kutumia lugha hiyo kimataifa kwa ajiri ya kuongeza ajira

Mhe Kasim Majarilwa akijibu swali hilo alifafanua kua serikali imeshaamua kua kiswahili ni lugha rasmi serikalini na hata bungeni huku lugha hiyo ikiwa miongoni mwa lugha rasmi katika jumuiya ya afrika mashariki

katika majibu yake alibainisha kwamba katika vyo vingi dunia wanafundisha Kiswahili hvyo ongezeko la waalimu wa kiswahili limekua likiongezeka na serikali imeakikisha kwamba katika vyuo vyetu nchini vinafundisha kiwsahili ili kukabiliana na fursa hiyo  ya ajira

0 comments:

Post a Comment