TCRa imefafanua aina ya simu zilizo fungiwa kupitia
meneja wa mawasiliano wa TCRA ndungu Innocent Mungy
Tukizungumzia ambavyo vimezimwa kinachofanyika kuzifunga
zile IMEI bandia ambazo kwa jana tumefanikiwa kuzifunga simu zenye IMEI
zipatazo laki sita na elfu 3 kwa maana ya kwamba unakuta simu moja ina IMEI
mbili kwasababu simu yenye laini mbili ina IMEI mbili sasa ziko simu zenye IMEI
hadi nne‘- Innocent Mungy
Kwahiyo ambacho tumeblock jana usiku ni IMEI laki sita
ikiwa ina maana ni ambazo zinatumika kwenye simu feki, modem ya internet na
IPAD, sasa sisi hatuwezi kutaja idadi ya simu ngapi tumezifungia ila tunachokijua
ni kwamba IMEI laki sita ndio zimefungiwa zilizopo kwenye simu‘– Innocent Mungy
‘Zoezi hili bado linaendelea ambapo sasa hivi mtambo
utakuwa unahakikisha simu zinazoingia bandia zitakuwa zinafungiwa, IMEI ni
namba tambulishi kama unakumbuka tulisema kwamba kila simu inayotengezwa
inapewa namba tambulishi, sasa simu ili itengenezwe lazima ipite kwenye
mchakato wa kuhakikisha kuna vitu ambavyo havitakiwi viwepo kwenye simu- Innocent
Mungy

0 comments:
Post a Comment